Lamentations 1:1-6

1 aTazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa,
mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu!
Jinsi ambavyo umekuwa kama mama mjane,
ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa!
Yule ambaye alikuwa malkia miongoni mwa majimbo
sasa amekuwa mtumwa.


2 bKwa uchungu, hulia sana usiku,
machozi yapo kwenye mashavu yake.
Miongoni mwa wapenzi wake wote
hakuna yeyote wa kumfariji.
Rafiki zake wote wamemsaliti,
wamekuwa adui zake.


3 cBaada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili,
Yuda amekwenda uhamishoni.
Anakaa miongoni mwa mataifa,
hapati mahali pa kupumzika.
Wote ambao wanamsaka wamemkamata
katikati ya dhiki yake.


4 dBarabara zielekeazo Sayuni zaomboleza,
kwa kuwa hakuna yeyote anayekuja
kwenye sikukuu zake zilizoamriwa.
Malango yake yote yamekuwa ukiwa,
makuhani wake wanalia kwa uchungu,
wanawali wake wanahuzunika,
naye yuko katika uchungu wa maumivu makuu.


5 eAdui zake wamekuwa mabwana zake,
watesi wake wana raha.
Bwana amemletea huzuni
kwa sababu ya dhambi zake nyingi.
Watoto wake wamekwenda uhamishoni,
mateka mbele ya adui.


6 fFahari yote imeondoka
kutoka kwa Binti Sayuni.
Wakuu wake wako kama ayala
ambaye hapati malisho,
katika udhaifu wamekimbia
mbele ya anayewasaka.

Copyright information for SwhKC